Loading...

MJUE MWANAMKE ANAYEOGELEA KATIKA MAJI YA BARAFU ILI KUZUIA KUZEEKA

Loading...
Inna Vladimirskaya (32) kutoka Kiev, Ukraine amejikuta akijiingiza katika ibada ya ajabu ambapo alidai inamsaidia asizeeke na kuwa mwenye afya.

Mwanamke huyo wa Ukraine huogelea katika mto wenye maji baridi huko Ulaya na kufanya mazoezi ya kukimbia kila mwisho wa juma wenye jotoridi la hasi -9C.

Mke wa Vladimirskaya, anakimbia akiwa mtupu katika kingo za mto Dnieper, huko Kiev, kila Jumapili, na anaogelea baada ya kumaliza kupasha mwili kwa kufanya mazoezi ya viungo.
Kwa mujibu wa Daily Mail, amekuwa akifanya hivyo kwa kipindi cha miaka 9 sasa, na muda mwingi anasindikizwa na mumewake.

Picha zake hizo za utupu ziliripotiwa kupigwa na mpiga picha David Tesinsky kutoka Czech, ambaye iliripotiwa kamba alisikia taarifa hizo za ibada ya huyo mwanamke kutoka kwa wakazi na kuamua kwenda kumpiga picha.

Akizungumza na DailyMail, alisema: "Kila wiki nakimbia katika mabarafu na kuoga katika ya baridi. Kuzama katika maji ya baridi kunafanya damu iweze kutembea katika ogani za ndani ya mwili, kunaamsha mzunguko, ambao unasaidia kuyeyusha mafuta na kuimarisha misuli.

"Pia inasaidia kumaliza maumivu ya misuli na viungo na kunawirisha ngozi yangu, kwa sababu ya kuongezeka usambazaji wa hewa safi ya oxygen ndani yake. Walrus anaonekana mtoto zaidi kuliko umri wake, kwa sababu hutumia muda mwingi akiwa katika maji ya baridi.

"Binadamu anaweza kupata faida hiyo hiyo kama wakijiandaa na kazi ya ziada. Na nahakikisha sikai katika maji kipindi kirefu , na mara tu nikitoka katika maji najikausha na kuingia katika gari langu lenye joto," Alisema. Picha zaidi...
Na Peter Godwin - Dar es salaam.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afya punde zinapojiri.
MJUE MWANAMKE ANAYEOGELEA KATIKA MAJI YA BARAFU ILI KUZUIA KUZEEKA MJUE MWANAMKE ANAYEOGELEA KATIKA MAJI YA BARAFU ILI KUZUIA KUZEEKA Reviewed by By News Reporter on 3/18/2018 10:43:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.