Loading...
Kwa mujibu wa Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria Tanzania 2017 uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na kuzinduliwa leo tarehe 25 Aprili 2018 mjini Kasulu Kigoma kiwango cha maambukizi ya Malaria nchini Tanzania kimeshuka kwa zaidi ya nusu kutoka asilimia 14.4 (2015) hadi asilimia 7.3. Mafanikio haya yametokana na mipango na mikakati mizuri iliyowekwa na Serikali ya Awamu ya 5 inayoongozwa na Dr John Pombe Magufuli ya kuhakikisha kuwa malaria inadhibitiwa na hatimae inatokomezwa nchini Tanzania.
Hata hivyo, bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Mikoa 10 kati ya 26 ya Tanzania Bara ina viwango vikubwa vya maambukizi ya malaria. Hii ni Kigoma (24.4%), Geita (17.3%), Kagera (15.4%) Mtwara (14.8%), Ruvuma (11.8%), Lindi (11.7%), Tabora 11.7%, Mara - 11.2%, Morogoro - 9.5% and Mwanza - 8.9%
Nitoe wito kwa kila mmoja wetu kuchukua hatua ili tuweze kutokomeza Malaria nchini ikiwemo kusafisha mazingira yetu, kufukia mazalia ya mbu na unyunyiziaji dawa za kuua viluwiluwi. Aidha kila mtu mwenye dalili za Malaria awahi au asaidiwe kuwahi kwenye vituo, apimwe na kupata tiba sahihi kwani Sio Kila Homa ni Malaria. Kumbuka - Kipimo cha haraka cha malaria (mRDT), dawa mseto ya Malaria na sindano ya Malaria kali (Artesunate) kuwa zinatolewa BURE katika vituo vyote vya kutolea huduma vya Serikali.
Niendelee kusisitiza kuwa jukumu la kutokomeza Malaria nchini ni la kila mmoja wetu. Kwa upande wetu, Serikali ya Awamu ya 5 itahakikisha Maafisa Afya katika Halmashauri zote nchini wanaamka na kutimiza majukumu yao ipasavyo katika kusimamia Afya na Usafi wa Mazingira. Pia tutahakikisha wajawazito wote nchini wanapata Dawa-kinga ya malaria SP kwa vipindi maalum wakati wa ujauzito wao ili kuwakinga malaria.
Aidha, tumeamua kuanzia mwaka wa fedha 2018/19 kukata Asilimia 3 ya fedha za dawa nchi nzima ili kununua viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi vya mbu na kuvisambaza kwenye Mikoa 10 yenye maambukizi makubwa.
#TanzaniaBilaMalariaInawezekana!
Mimi niko tayari kutokomeza Malaria wewe je?
Ummy Mwalimu,Mb
WAMJW
25.April 2018

KIWANGO CHA MAAMBUKIZI YA MALARIA NCHINI CHAPUNGUA
Reviewed by By News Reporter
on
4/25/2018 10:12:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: