Loading...
Maandamano hayo yanafanyika wakati ambapo ripoti ya uchunguzi uliyoagizwa na waziri wa afya nchini humo inatarajiwa kutolewa rasmi.
Waziri wa afya nchini Kenya Dkt Cleopha Mailu aliagiza uchunguzi kufanywa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta baada ya wanawake waliojifungua kudai kwamba wanadhalilishwa kingono.
![]() |
Wanawake 100 hujifungua kila siku hospitali ya Kenyatta. |
Taarifa zilizoenezwa kwenye mitandao siku ya Ijumaa zinadai kina mama waliojifungua wamekuwa wanashambuliwa na baadhi ya wafanyikazi wakati wakienda kwenye chumba cha watoto wachanga kuwanyonyesha watoto wao.
Wanaotuhumiwa ni wahudumu katika vyumba vya maiti, wanaonyooshewa kidole pia kwa kutumia maiti kuwashutua akina mama waliojifungua katika hospitali hiyo.
![]() |
Waandamanaji wamemiminika mjini Nairobi kuitaka serikali ichukuwe hatua dhidi ya tuhuma za ubakaji katika hospitali |
Wanaharakati wa kutetea haki za wanawake wanaoandamana leo katika mji mkuu, wanasema dhamira yao kuu kumiminika barabarani ni kutaka mabadiliko yafanyike, na kwamba usalama wa wanawake ni jambo linalopaswa kutiliwa umuhimu.
Mildred Atty ni mojawapo ya waandalizi wa maandamano hayo.
Katika mahojiano na BBC amesema, 'limekuwa likiendelea kwa muda usiojulikana, na ni lazima liishe'.
Hospitali ya taifa ya Kenyatta, Nairobi huwahudumia kina mama takriban 100 wanaojifungua kila siku.
Watoto waliozaliwa huwekwa chumbani ghorofa ya kwanza nao wanawake kwenye wodi za kujifungulia kwenye ghorofa ya chini.
Maswali sasa yameanza kuulizwa kuhusu muundo na mpangilio wa vyumba katika hospitali hiyo ambao huwalazimu kina mama waliojifungua kupanda ngazi au lifti kwenda kuwanyonyesha watoto wao, ikizingatiwa kwamba baadhi hujifungua kupitia upasuaji.
source: BBCSWAHILI
Madai ya Ubakaji katika Hosipitali ya Kenyatta yazua Maandamano - Kenya
Reviewed by By News Reporter
on
1/23/2018 03:58:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: