Loading...

MAMBO YA KUFANYA ILI KUJENGA TABIA YA KUCHUKUA HATUA KWA VITENDO - Na Siri ya Utajiri

Loading...

Yafuatayo ni mambo ambayo yatakusaidia kujenga tabia ya kuchukua hatua kwa vitendo:-

1. Thubutu kujaribu, usiogope kujaribu.

2. Usisubiri mambo yote yakae sawa,hakuna siku kila kitu kitakaa sawa.

3. Kuwa na ujasiri wa kufanya kile unachokiogopa, ukishaanza kukifanya tu hofu yote inapotea.

4. Anza leo , usiruhusu kusema utaanza kesho au wiki ijayo au mwaka ujao. Kufanya hivyo unakaribisha kushindwa.

5. Usitumie muda mwingi sana kujiandaa kufanya jambo, anza hivyo hivyo kwa kutumia hicho hicho ulichonacho.

6. Usiogope watu wengine watasema nini au watakuonaje.

Kuwa na mawazo na mipango mizuri pekee haikusaidii kitu, ili uweze kupata manufaa kutoka katika mawazo hayo lazima uchukue hatua kwa vitendo.

You Deserve The Best!
Vicent Stephen

MAMBO YA KUFANYA ILI KUJENGA TABIA YA KUCHUKUA HATUA KWA VITENDO - Na Siri ya Utajiri MAMBO YA KUFANYA ILI KUJENGA TABIA YA KUCHUKUA HATUA KWA VITENDO - Na Siri ya Utajiri Reviewed by By News Reporter on 1/28/2018 06:54:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.