Loading...

BABA "AWABAKA WATOTO WAKE MAPACHA NA KUWAFUNGA MNYORORO KWA KIPINDI CHA MIAKA KUMI"

Loading...
Baba mmoja ameshtakiwa kwa kuwabaka watoto wake wa kike mapacha mara kwa mara na kuwashindisha njaa kwa kipindi cha miaka 10.

Jerry Lee Curry (51), ameshukiwa kwa kuwafunga mnyororo binti zake kwa kipindi cha miaka 10, huku akiwashindisha njaa na kuwapiga kwenye nyumba yake huko Minneapolis, Minnesota, Marekani. Baba huyo aliwatesa binti zake kwa miaka mingi, akiwafunga na mnyororo na kuwapa chakula kidogo. Na kusababisha watoto hao kupata majereha kadhaa ya muda mrefu na kuathirika kiakili.

Muathirika mmoja wapo ameumia vibaya eneo la sikio na alikutwa na kovu eneo la kichwa na mgongoni. Alisema baba yao alimpiga na gongo.

Uteswaji huo wa watoto hao wa kike uliendelea na kutogunduliwa kwa muda wote wa miaka 10 mpaka pale mmoja wa watoto hao kutoroka na kwenda kupata msaada wa polisi. Kwa mujibu wa mtandao wa Star Tribune, mmoja wa mabinti hao alisema unyanyasaji huo wa kijinsia waliofanyiwa ulianza pale walipogundulika wamebalehe.

Aliongezea: "Alinilazimisha kufanya mapenzi nae, na alinifanya kila siku tangu nikiwa mdogo wa miaka 10. Alifanya hivyo kwa mdogo wangu pia."

Mabinti hao sasa wanamiaka 20, na wanaumwa magonjwa ya kisaikolojia.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Kimataifa punde zinapojiri.
BABA "AWABAKA WATOTO WAKE MAPACHA NA KUWAFUNGA MNYORORO KWA KIPINDI CHA MIAKA KUMI" BABA "AWABAKA WATOTO WAKE MAPACHA NA KUWAFUNGA MNYORORO KWA KIPINDI CHA MIAKA KUMI" Reviewed by By News Reporter on 2/24/2018 12:16:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.