Loading...

NAY WA MITEGO: MIMI NDIO CHANZO CHA NYIMBO ZA WASANII WENGINE KUFUNGIWA

Mwanamuziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki, alimaarufu kama Ney wa Mitego amesema yeye ndio chanzo cha nyimbo za wasanii wengine kufingiwa.

Nyimbo zaidi ya kumi zilitangazwa na Mamlaka ya Mawasiliano kupigwa marufuku kuchezwa katika radio nchini.

Ney wa mitego akiongea chombo kimoja cha habari,amesema

'Wakati mwingine naona kuwa sababu ya kufungiwa kwa miziki hii ni mimi na wengine wanawekwa kama chambo kwa kuwa kati ya nyimbo zote hizo,nyimbo mpya peke yake ni yangu tu ambayo imetoka wiki mbili zilizopita na video ina wiki moja tu" Ney wa Mitego.

Loading...
n: center;"> Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa mwanamuziki huyo kupata misukosuko katika muziki wake.

Mnamo mwezi machi mwaka jana Ney wa Mitego aliwahi kukamatwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuimba wimbo unaokashifu serikali lakini inakumbukwa kuwa mwanamuziki huyo aliwahi kupewa onyo kuhusiana na mavazi yake.

Huku wanamuziki wengine bado hawakuwa tayari kutoa maoni yao.

Wakati huo huo , hii leo, msanii wa bongo fleva, Roma Mkatoliki aliyefungiwa wimbo wake mpya wa 'kibamia' kwa sasa amefungiwa na Naibu Waziri wa habari,sanaa,utamaduni na michezo Juliana Shonza kutojihusisha na tasnia ya muziki kwa takribani miezi sita mara baada ya kukiuka kurekebisha wimbo huo.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
NAY WA MITEGO: MIMI NDIO CHANZO CHA NYIMBO ZA WASANII WENGINE KUFUNGIWA NAY WA MITEGO: MIMI NDIO CHANZO CHA NYIMBO ZA WASANII WENGINE KUFUNGIWA Reviewed by By News Reporter on 3/01/2018 10:08:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.