Kuna mazingira fulani ambapo kuna UTARATIBU uliokubalika, kwamba ukitaka kufanya jambo fulani unashauriwa upitie utaratibu huo ambao wengine wengi wameutumia kuweza kufanikisha jambo hilo.
Katika hali hii kumekuwa na UKOMO wa MAFANIKIO katika mambo hayo kwa sababu watu wanafanya kadri ya utaratibu ulivyo.
Kwa wewe pia unayetaka kufanya jambo lililo ndani ya utaratibu fulani kumbuka kitu kimoja. Kama unataka kufanikiwa zaidi ya kiwango walichofikia wengine usitosheke kwa kufanya kadri ya utaratibu uliotengenezwa. Fanya zaidi ya kile kilichoainishwa katika utaratibu.
Loading...
xt-align: left;">
Hapa namaanisha kuwa na MTAZAMO chanya wa kufikri zaidi, kuwa MBUNIFU zaidi ya kile kilichopo, kuwa na mtazamo wa KUBORESHA zaidi ya utaratibu uliopo. Usikubali utaratibu ulioukuta ndio uwe MWISHO wa fikra zako, muda wote tafuta namna ya kupanua WIGO kwa kuboresha.
Kwa kufanya hivi utajitofautisha na wengine na utafanikiwa zaidi ya wenzako.
You Deserve The Best!
Vicent Stephen
Tuma neno 'MAKALA' kwenda +255765112259 kupata muendelezo wa makala punde zinapojiri.
USIKUBALI KUWA WA KAWAIDA JARIBU KUWA MBUNIFU - Na Siri ya Utajiri
Reviewed by By News Reporter
on
3/02/2018 05:50:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: