Loading...
Dodoma, imeripotiwa kuwa na namba kubwa ya wagonjwa wa kipindupindu kwa kipindi cha miezi mitatu toka mwaka uanze, ikiongoza mikoa yote.
Ripoti hiyo ilitolewa na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Bi Ummy Mwalimu alisema idadi ya wagonjwa iliyoripotiwa kwa mkoa huo inafikia asilimia 40 ya wagonjwa wote nchi nzima.
Wakati wa kutoa ripoti hiyo, iliripotiwa kwamba kuna jumla ya wagonjwa 1448 nchi nzima na 583 kati yao waliripotiwa kutokea Dodoma na waliofariki ni 27 mpaka sasa.
Ruvuma ni mkoa wa pili ambapo jumla ya kesi 374 zimejitokeza au 25% ya wagonjwa wote nchini wakati Rukwa na Iringa ni kesi 276 (sawa na 19 asilimia) na 88 (6.1 asilimia) kwa mfuatano.
Manyara ndio ina idadi ndogo ya wagonjwa wa kipindupindu, ambayo ni 0.6 asilimia kwa wagonjwa wote.
"Ripoti inaonyesha idadi ya vifo vya wagonjwa wa kipindupindu imepngua ukilinganisha na hapo nyuma. Ijapokuwa Dodoma imekuwa ikiogopesha, " waziri alisema.
Ummy Mwalimu alisisitiza kwamba usafi wa mazingira lazima uzingatiwe.
Na Geofrey Okechi.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afya punde zinapojiri.

WAGONJWA WA KIPINDUPINDU 'DODOMA' YAONGOZA ORODHA
Reviewed by By News Reporter
on
4/10/2018 06:30:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: