Loading...
Diamond Platinumz hivi kupitia mtandao wake wa Instagram amethibitisha kwamba yuko katika mahusiano ya kimapenzi na mrembo Mkenya kwa kurusha kipande cha video kilicho waonyesha wapo katika mahaba mazito maeneo ya ufukweni.
Mwanadada huyo kwa jina kamili anaitwa Natasha Dona Okechi na ni raia wa Kenya, ambaye anajishughulisha na kazi za utangazaji katika kituo cha radio cha NRG na pia ni video vixen na mwanamitindo wa muda mrefu ambaye alifanya video kama 'Nagharamia' ya Christian Bella aliyomshirikisha Alikiba.
Ni chotara aliyezaliwa na wazazi wenye asili mbili Kenya na Italia, alizaliwa nchini uingereza lakini alihamia Kenya baadae akiwa na umri wa miaka 11.
Tanasha alishapata skendo ya kutoka na AliKiba lakini alizipuuzilia mbali mwanzoni mwa mwaka huu.
Lakini mpaka sasa Tinasha bado hajazungumzia taarifa hizi za uhusiano baina ya wawili hao hadharani, jambo ambalo linazua maswali kuhusu kama ni kweli wapenzi au la. Lakini tutajua ukweli zaidi siku zitakavyozidi songa.
Na Haika Gabriel.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

DIAMOND ATIA NGATA KISIMA CHA ALIKIBA, MREMBO MKENYA AWAZUZUA?
Reviewed by By News Reporter
on
11/30/2018 10:17:00 AM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
11/30/2018 10:17:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: