Loading...

MENGI: BILA K-LYNN HUENDA NINGESHAFARIKI?

Loading...
Mmiliki wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi ameeleza jinsi alivyokutana na mlimbwende wa Tanzania mwaka 2001,  Jacqueline Ntuyabaliwe maarufu K-Lynn kwa mara ya kwanza jijini London, Uingereza mwaka 2010.

Akizungumza na kituo cha televisheni Citizen cha Kenya nyumbani kwake, Mengi amesema kama asingekuwa na mrembo huyo hadi sasa huenda angekuwa ameshafariki dunia.

Kinyume na watu wanavyofikiria anakiri kuwa haikuwa rahisi kumpata K-Lynn  na huenda yeye ni miongoni mwa watu walionufaika na mashindano ya Miss Tanzania.

Pia kupitia  kitabu cha 'I can I must I will', Mengi anamzungumzia mrembo huyo kama mtu aliye leta mwangaza katika maisha yake.

Kwa sasa Dr Mengi na K-Lynn wamebahatika kupata watoto wawili mapacha baada ya kufunga ndoa.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MENGI: BILA K-LYNN HUENDA NINGESHAFARIKI? MENGI: BILA K-LYNN HUENDA NINGESHAFARIKI? Reviewed by By News Reporter on 12/05/2018 07:40:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.