Loading...

MSANII NA RAPPA DMX ARUDISHWA JELA TENA

Loading...
Rappa DMX kushoto akiwa Mwandishi wa habari wa kituo cha FOX
DMX anarudi jela kwa kukuika jaribio lake katika kesi yake ya kukimbia kodi ambapo alikutwa na hatia mwezi uliopitwa kwa kukwepa kulipa kodi ya thamani ya dola za Kimarekani 1.7 milioni ambazo alikuwa akidaiwa. Rappa huyo alifikishwa mahakama ya Manhattan Jumanne asubuhi kwa kukaidi kufanya vipimo vya madawa ya kulevya.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, hakimu alisema rappa huyo alikuwa na hatari ya kukimbia baada ya kugundulika anamajibu chanya ya matumizi ya dawa za kulevya kama Opiates, cocaine na oxycodone. Sehemu ya masharti ya dhamana yake ni yeye kukaa mbali na matumizi ya madawa ya kulevya na pombe.

DMX alitakiwa kukamilisha rehab kipindi chote cha dhamana kwa kesi ya kukwepa kulipa kodi, na pia alipatiwa mpaka usafiri kwa ajili ya matamasha yake ya hivi karibuni lakini baada ya kushindwa kufanya majaribio yake ya madawa ya kulevya alirejeshwa jela.

Msemaji wa Mwanasheria wa Marekani Nicholas Biase anasema waendesha mashtaka walikiri kupitia video iliyorushwa na mtandao wa TMZ wiki iliyopita ya DMX, ambayo ilimwonyesha kama akiwa amelewa sana, huko katika baa moja katika uwanja wa ndege wa St. Louis, ambapo mashahidi walisema alikuwa akinywa na kuwanunulia wengine pombe kali. Ikiwa kunya pombe kali ni kukiuka masharti ya dhamana hiyo.

Dmx kwa sasa anasubiri hukumu yake mwezi Machi.
MSANII NA RAPPA DMX ARUDISHWA JELA TENA MSANII NA RAPPA DMX ARUDISHWA JELA TENA Reviewed by By News Reporter on 1/31/2018 07:48:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.