Loading...

"NITAPAMBANA NA RUSHWA BEGA KWA BEGA KWA MAENDELEO YA AFRIKA" - ASEMA RAIS GEORGE WEAH AKIWA AU, MKUTANO WA 30

Loading...
Rais wa Liberia George Weah, akiwa Addis Ababa - Mkutano wa 30 wa AU.
Seneta George Weah, Rais wa 24 wa Liberia alipoonekana kwa mara ya kwanza katika Umoja wa Afrika (AU), jumapili ya jana katika mkutano wa 30 wa umoja huo, na kusisitiza juhudi atakazoweka ili kupambana na rushwa kwa ajili ya maendeleo ya Afrika.

Akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa Mkutano huo wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Weah alisema kuwa: "Rushwa ni janga ambalo linaonekana kujitokeza katika nchi zetu zote na kujionyesha katika namna nyingi sana."

"Mimi na serikali yangu tutafaidika sana kutokana na majadiliano juu ya mada hii muhimu kama dhima muhimu zaidi katika mkutano huu - Kuzuia na Kupambana na rushwa: Kama njia endelevu ya Mabadiliko ya Afrika." Alisema Weah.
Rais George Weah, akiwasili Addis Ababa
Kwa mujibu wa Weah, Rusha ni adui wa maendeleo na ukuaji katika Sekta ya Uchumi wa Afrika. Pia alisema rusha imefanya kuwa ngumu kwa watu wa afrika kuufikia uwezo wao wa kweli na kamili.

Pia alionyesha matarajio yake kuwa jumuhia ya viongozi wa nchi za umoja wa Afrika na serikali zao wanapaswa kuonyesha za dhati ili kuhakikisha wanakabiliana changamoto zinazotokana na rushwa.

Weah, ambaye alisalimiwa na viongozi wenzake wa Afrika kwa kuonekana mara ya kwanza huko AU, pia aliapa kufanya kazi pamoja na nchi nyingine za Afrika kwa maendeleo ya pamoja.

"Nina hakika kwamba viongozi wenzangu ambao, kwa msaada na mwongozo wenu, nitaweza kutekeleza ahadi nilizohaidi kwa watu wangu wa Liberia, ahadi zilizolenga kupambana na umasikini na kujenga mazingira ya ambayo ndoto zao na matarajio yao kufikiwa" alisema Weah.

Natarajia kufanya kazi na nyinyi kama wote manavyojitahidi kudumisha amani katika bara hili ili kuendeleza usalama na utulivu ambapo nchi zetu zinalenga kukuza na kutaraji," aliongeza.
"NITAPAMBANA NA RUSHWA BEGA KWA BEGA KWA MAENDELEO YA AFRIKA" - ASEMA RAIS GEORGE WEAH AKIWA AU, MKUTANO WA 30 "NITAPAMBANA NA RUSHWA BEGA KWA BEGA KWA MAENDELEO YA AFRIKA" - ASEMA RAIS GEORGE WEAH AKIWA AU, MKUTANO WA 30 Reviewed by By News Reporter on 1/29/2018 07:59:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.