Loading...
Kushoto Rappa Jay-Z, kulia rais Trump |
Usiku wa juzi mwanamuziki nguli, Jay Z alikuwa mgeni katika show ya Van Jones kwenye CNN ambako alimshambulia kwa maneno rais kwa namna ya kuvutia.
Rappa huyo alisema, hata kama Jumuiya ya Waafrika Wamerikani wanafaidika katika uongozi wa rais Trump lakini kauli za rais huyo aziwapendezi masikioni mwao.
Kwa maneno yake, "Nitese sana na unilipe vizuri. Haiwezi kuzalisha furaha. Kila mtu atakuja kuwa dhaifu."
Bila kupoteza muda, Rais Trump alijibu kauli za rappa huyo kwa kutumia mtandao wa twitter jana jumapili akisema: "Naomba mtu amjulishe Jay Z kuwa kwasababu ya sera zangu, Ajira za watu weusi imeshuhudiwa kuongezeka kwa kiasi kubwa kuliko REKODI yeyote iliokwisha wekwa"
HII NDIO TWEET ALIYOANDIKA DONAL TRUMP
RAIS TRUMP AMJIBU JAY-Z KUPITIA MTANDAO WA TWITTER
Reviewed by By News Reporter
on
1/29/2018 08:46:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: