Loading...
![]() |
| Filamu ya Watu wote. |
Filamu kuhusu shambulizi la kigaidi la Alshabaab nchini Kenya ambapo watu 2 waliuawa ndani ya basi eneo la Mandera mwaka 2014 imeteuliwa kushindania tuzo maarufu za Oscar mwaka huu huko nchini Marekani.
Filamu hiyo ilikuwa imeshinda tuzo za Oscar kitengo cha wanafunzi mwaka jana na kuwa filamu ya kwanza kutoka Kenya kushinda tuzo hiyo.
Filamu hiyo ya Watu Wote imeorodheshwa kushindania kitengo cha Filamu Bora Fupi: Matukio Halisi.
Itashindana na filamu nyingine nne ambazo ni "Dekalb Elementary", "The Eleven O'Clock", "My Nephew Emmett" na "The Silent Child".
Filamu hiyo inayoeleza hadithi ya Kenya, kuhusu Wakenya na inashirikisha waigizaji wa Kenya, inasimulia shambulio hilo la mwaka 2014 kaskazini mwa Kenya, ambapo maudhui ya uadui wa kidini kati ya Wakristo na Waislamu yanaangaziwa.
Ni mara ya kwanza ambapo filamu ya kenya imeteuliwa kuwania tuzo ya Oscars. Lakini ni mara kadhaa wasanii wa filamu kutoka Kenya kuwania tuzo kubwa na wengine hata kushinda tuzo hizo, kwa mfano muigizaji Lupita Nyong'o ambaye alishinda tuzo za BET Award kama muigizaji bora wa kike katika filamu ya '12 years of slave'.
Hii inaonyesha Kenya sasa imepiga hatua katika soko la filamu hapa Afrika Mashariki ukilinganisha na nchi za jirani kama Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.
WAKENYA WANG'ARA TUZO ZA OSCAR NCHINI MAREKANI
Reviewed by By News Reporter
on
1/27/2018 12:33:00 AM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
1/27/2018 12:33:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: