Loading...
Mzee Kingunge enzi za uhai wake. |
Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Kingunge Ngombale-Mwiru, 87, amefariki dunia.
Mzee Kingunge amekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mwanasiasa huyo mkongwe alilazwa hospitalini mwanzoni mwa Januari akiuguza majeraha ya kushambuliwa na kung'atwa na mbwa nyumbani kwake na akafanyiwa upasuaji.
Alikuwa mmoja wa viongozi wa muda mrefu na miongoni wa watu waliokuwa na ushawishi katika Chama cha Mapinduzi (CCM) hadi alipojiuzulu kutoka kwenye chama hicho Oktoba 2015 akilalamikia alichosema ni ukiukaji wa katiba ya chama hicho.
Kabla ya kujiuzulu, alikuwa amesema kwamba hakuwa amefurahishwa na utaratibu uliotumiwa kumteua mgombea urais wa CCM mjini Dodoma Julai mwaka huo.
Hata hivyo, aliahidi kutohamia chama kingine.
Bw Kingunge alikuwa amehdumu katika CCM tangu kuanzishwa kwa chama hicho mwaka 1977.
Mke wake, Peras, alifariki dunia mwezi uliopita akitibiwa pia Muhimbili baada ya kulazwa kwa miezi kadha.
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli alikuwa amefika katika Wodi ya Mwaisela iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kumjulia hali Mzee Kingunge mwanzoni mwa mwezi Januari.
"MUNGU AILAZE ROHO YA MZEE WETU MAHALI PEMA PEPONI AMEN"
BREAKING NEWS: MZEE KINGUNGE NGOMBALE-MWIRU AFARIKI DUNIA
Reviewed by By News Reporter
on
2/02/2018 07:16:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: