Loading...

MASWALI MAZURI YA KUMUULIZA MPENZI WAKO SIKU YA VALENTINE DAY!

Loading...
Wakati unaingia katika mahusiano mapya na mtu, unapaswa kujua mengi kuhusu yeye, na maswali kadhaa utakayomuuliza yatakujulisha mengi kuhusu yeye.

Yafuatayo ni maswali unayopaswa kumuuliza mpenzi siku hii maalamu kwa wapenda nao:-
1. FAMILIA YAKO IPOJE NA INAFANANAJE?
Hii itakujulisha kujua mahusiano yaliyopo kati ya huyo mtu na familia yake; kama ni kijana anayeangalia mbele kuwa na familia yake au la. Familia zetu zinatuathiri kwa kiasi kikubwa sana na historia ya familia yake itakuonyesha huyo ni mtu wa namna gani.

2. MAHUSIANO YAKE YA NYUMA
Sio kwamba umevutiwa na mpenzi wake wa zamani lakini kujua mahusiano yake ya nyuma itasaidia sana. Itasaidia kujua yeye kijana wa namna gani katika mahusiano.

3. NINI ANATAKA KATIKA MAHUSIANO?
Kila mtu kipo anachohitaji katika mahusiano na kipo katika akili yake watu wengi wanataka vitu tofauti. Hii itaonyesha mahusiano yana maana gani kwake.

4. MWANAMKE WAKO YUPOJE?
Wanaume tofauti wanataka vitu tofauti kwa wanawake; kitakacho kuwa kizuri kwa Juma kama hakiwezi kizuri kwa Geofrey. Kujua ni anataka mwanamke wa namna gani itakusaidia kama upo katika upande anaoutaka.

5. NINI UNAPENDELEA KUFANYA?
Anachopenda kufanya mtu kinaonyesha yeye ni mtu wa namna gani; Kama ni anapenda utalii, kama ni anapenda kuogelea au anapenda michezo.

6. JE UNAPENDA KUWA NA MAHUSIANO NA BIKIRA?
Amini hiki, sio kila mwanaume anampenda bikira na sio kila mwanaume atamkubali asiyekuwa na bikira, wanaume wengine wanapenda mwanamke mwenye ubikira lakini wengine hawapendi.

7. JE ANAMSIMAMO GANI KATIKA KUFANYA MAPENZI MPAKA TUOANE?
Ni kijana ambaye atasubiri katika hilo, na kama hautohitaji kufanya mapenzi atakuwa tayari kusubiri hilo au atakulazimisha katika mfanye. Swali hili litakusaidia kutambua hilo.

8. JE UTAKUWA MWAMINIFU?
Kuwa na mahusino ya kimapenzi na mwanamke asiyetaka kufanya mapenzi, ataendelea kuwa mwaminifu na asikusaliti na kufanya mapenzi na msichana mwingine.

9. NINI MALENGO YAKO KATIKA MAISHA?
Ni vizuri kujua malengo ya mwanamume wake na ndoto za maisha yake, mtazamo juu ya maisha yake ya baadae na jitihada anazofanya kuhakikisha anazifikia.

10.  UNAJIONA WAPI BAADA YA MIAKA MITANO (5)?
Haya ni malengo ya muda mfupi zaidi ukilinganisha swali lililopita. Swali hili litaonyesha malengo ya muda mfupi na maono.
MASWALI MAZURI YA KUMUULIZA MPENZI WAKO SIKU YA VALENTINE DAY! MASWALI MAZURI YA KUMUULIZA MPENZI WAKO SIKU YA VALENTINE DAY! Reviewed by By News Reporter on 2/12/2018 07:37:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.