Loading...

POLISI CHINA KUKAMATA WAHALIFU KUTUMIA TEKNOLOJIA YA MIWANI

Loading...
Ofisa Polisi akiwa amevaa miwani za kuwakamatia wahalifu.
Polisi nchini China wameanza kutumia miwani za jua zenye uwezo wa kutambua sura za watu wanaotuhumiwa kwa uhalifu. Vyoo vya miwani hizo vimeunganishwa mfumo wa utunzaji wa taarifa za wahalifu wote, ikimaanisha maafisi polisi wanauwezo wa kutafuta haraka haraka katika halaiki ya watu na kuwakamata mara moja.

Wahalifu ijapokuwa wanahofu na teknolojia itawaongezea serikali nguvu zaidi ya kupambana na wahalifu lakini miwani hizo za jua tayari zimeshaidia polisi hao kukamata watuhumiwa saba (7), kwa mujibu wa vyombo vya habari vya China.

Katika jiji la Zhengzhou karibu na kituo cha usafiri wa treni. Watu 7 walikamatwa waliotuhumiwa kwa makosa ya uporaji.

Polisi pia kwa kutumia teknolojia hiyo waliwatambua watu 26, waliokuwa wanatumia vitambulisho batili, gazeti la People Daily liliripoti.

Teknolojia hiyo inawaruhusu maofisa wa polisi kuchukua picha za raia katika makundi ya watu na kufananisha picha hizo na mfumo wa utunzaji taarifa za wahalifu na ikikuta zilizofanana na wahalifu, inatuma taarifa kama jina la muhalifu na mahali anapoishi kwa afisa.
POLISI CHINA KUKAMATA WAHALIFU KUTUMIA TEKNOLOJIA YA MIWANI POLISI CHINA KUKAMATA WAHALIFU KUTUMIA TEKNOLOJIA YA MIWANI Reviewed by By News Reporter on 2/12/2018 08:22:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.