Loading...
Dubai hawatanii linapokuja swala la maendeleo na ujenzi wa majengo marefu ya daraja la kwanza duniani.
Jiji kubwa katika Jumuia za nchi za Kiarabu ya Emirate linajenga mnara ambao utakuwa jengo refu duniani. Jengo hilo, wakati likikamilika, litakuwa na urefu wa futi 3,045, na kuzidi jengo refu duniani kwa futi 328, ambalo ni Burj Khalifa linaloshikilia rekodi kwa sasa. Jengo hilo linajengwa Kivuko cha Bandari ya Dubai.
Jengo hilo litakuwa na garden za wazi na kuwa na ghorofa kadhaa za wapangaji wa nyumba za makazi na maeneo ya kupangisha wafanya biashara. Jengo hilo libuniwa na msanii wa majengo Santiago Caltrava raia wa Hispania-Uswizi ambaye amebuni majengo maarufu duniani kote.
Jengo hilo limemebuniwa kwa teknolojia ya juu zaidi na linauwezo wa kujilinda thidi ya upepo na matetemeko.
Ujenzi wa mnara ulianza Oktoba 2016 na unatarajiwa kumalizika 2020. Na mradi unakadiriwa kutumia pesa za kimarekani dola bilioni 1, sawa na pesa za kitanzania zaidi ya tilioni 2.
DUBAI KUJENGA JENGO REFU KULIKO YOTE DUNIANI
Reviewed by By News Reporter
on
2/17/2018 08:17:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: