Loading...

TUMKUMBUKE BOB MARLEY KWA SIKU YAKE YA KUZALIWA - FEBRUARI 6

Loading...
Siku kama ya leo alizaliwa Mfalme wa muziki wa Raggae maarufu kama Bob Marley, na alizaliwa Nine Mile, Jamaica mwaka 1945 na hatimaye alifariki Mei 11, 1981.

Historia yake kwa ufupi:
Nesta Robert Marley aka Bob Marley, alijulikana kama balozi wa nchi za Dunia ya Tatu kwa muziki alioufanya na aliuza jumla ya nakala milioni 75 za Reggae duniani kote. Alikufa kwa ugonjwa wa saratani katika hospitali ya Cedars ya Lebanon huko Miami, Florida.

Kabla ya umaarufu:
Pamoja na uchotara wake lakini alitambulika kama Muafrika na alikuwa akiunga mkono harakati za Turudi Afrika na Rastafari. Alipendelea kubandika matangazo ya picha za Black Panthers na CheGuevera katika maduka ya Wailers Soul Shack Record.

Umaarufu wake:
Alitamba na vibao kama "No Woman, No Cry," "Could You Be Loved," "Get Up, Stand Up," na "Redemption Song" kabla ya kukikabili kifo chake cha kushangaza. Alizikwa na mpira wa miguu, Gitaa, Biblia na Puli la bangi. Mwaka 1994 aliingizwa Rock and Roll Hall of Fame.

Maisha ya familia:
Alimuoa Rita Marley Februari 10, 1966 na walibahatika kupata watoto wa tano (5). Alikuwa na jumla ya watoto kumi na moja (11) katika maisha yake yote ya mahusiano.

Alishafanya kazi na wasanii kama Peter Tosh, na Bunny Wailer na wakaunda kundi la The Wailers (Baadae Marley na The Wailers) mnamo mwaka 1963.

TUMKUMBUKE BOB MARLEY KWA SIKU YAKE YA KUZALIWA - FEBRUARI 6 TUMKUMBUKE BOB MARLEY KWA SIKU YAKE YA KUZALIWA - FEBRUARI 6 Reviewed by By News Reporter on 2/06/2018 05:10:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.