Loading...

HESHIMA ILIOJE, GAVANA MMOJA NCHINI NIGERIA APIGA GOTI AKISALIMIANA NA RAIS BUHARI

Loading...
Gavana El Rufai alionekana kupiga goti wakati akisalimiana na rais wa nchi yake ya Nigeria katika jiji la Kaduna.

Mapema leo, Rais Muhammadu Buhari alitembelea jiji la Kaduna katika uzinduzi wa Ndege ya kijeshi ya TSAIGUMI maarufu kama gari ya angani isiyo na rubani.

Rais alipokelewa na gavana wa jimbo hilo, Nasir El-Rufai ambaye alimsalimia kwa heshima na taadhima kwa kuinama chini kidogo ikiwa ni ishara ya kupiga goti.

Rais Buhari amezindua ndege hiyo inayojiendesha yenyewe bila ya rubani ambayo ni ya kwanza kutengenezwa nchini humo.

Kifaa hicho kilichotengenezwa na Taasisi ya Teknolojia ya jeshi la anga la Nigeria, kitatumika kupambana na wapiganaji pamoja na majambazi.

Mipango ya jeshi la nchi hiyo ni kutengeneza vifaa hivyo kwa wingi na pia uwezekano wa kuvisafirisha katika nchi nyingine.


Nigeria imekuwa ikikabiliwa na kitisho cha usalama, ikiwemo wapiganaji wa kiislamu walioko kaskazini mwa nchi hiyo, wapiganaji walioko katika eneo lenye utajiri wa mafuta, kusini mwa nchi na mapigano kati ya wafugaji na wakulima katika jimbo la kati mwa nchi hiyo.
HESHIMA ILIOJE, GAVANA MMOJA NCHINI NIGERIA APIGA GOTI AKISALIMIANA NA RAIS BUHARI HESHIMA ILIOJE, GAVANA MMOJA NCHINI NIGERIA APIGA GOTI AKISALIMIANA NA RAIS BUHARI Reviewed by By News Reporter on 2/16/2018 10:10:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.