Loading...
J.Lo akiwa na mpenzi wake Alex Rodriguez |
Kwa mujibu wa habari zilivyotufikia, uvumi huo ulianza baada ya chanzo kimoja kilichopo karibu na wapendanao hao walisema kuwa "Wapo karibu sana na wanazungumzia ndoa", akiongezea "J.Lo anamalengo na A-Rod."
Na baada ya kuzungumza nao hivi karibuni, walionekana wakitoa hisia sawa katika swala hilo.
J. Lo aliulizwa nini kinachokufanya umuone Rodriguez ndio chaguo lako, Lopez alisema, "Kwasababu ni yeye, na pia ananipa msaada sana katika shughuli zangu hata iwe usiku sana ataniunga mkono tu na cha mwisho anapenda ninachofanya, unajua kuwa na mtu anayeelewa unachofanya na kupenda kuwa karibu yako wakati unafanya hicho kitu inasisimua sana."
Chanzo hicho cha karibu kiliongeza mnamo Septemba 2017, walimuuliza Rodriguez kama angelikwepa swali hilo, na alisema, "Jennifer ni wa ajabu sana. Ni mzuri. Ananifanya niwe na furaha muda wote."
Hata hivyo, inaonekana vyombo vya habari na mashabiki wanawashawishi kuchukua hatua inayofuta ya kufunga NDOA.
JENNIFER LOPEZ NA MPENZI WAKE ALEX RODRIGUEZ NDOA INANUKIA
Reviewed by By News Reporter
on
2/02/2018 10:38:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: