Loading...
Mbunge wa makadara George Aladwa ni mwanasiasa wa tatau wa upinzani kukamtwa na maafisa wa polisi tangu kiongozi wa upinzani Raila Odinga alipojiapisha. |
Mbunge mwingine nchini Kenya, amekamatwa kuhusiana na mzozo unaozunguka kujiapisha kwa aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kwa kile anachokitaja kama rais wa watu wa Kenya.
Mbunge wa Makadara jijini Nairobi Goerge Aladwa amekamatwa asubuhi ya leo nyumbani kwake na maafisa wa idara ya upelelezi na kupelekwa hadi makao makuu ya idara hiyo kwa mahojiano zaidi.
Aladwa ambaye amewahi kuwa meya wa jiji la Nairobi, alikuwa katika mstari wa mbele katika mipango ya sherehe hizo ambazo hazikuwa na idhini ya serikali.
Aladwa sasa ni mbunge wa pili kukamatwa kuhusiana na hafla hiyo ambayo pia imeshutumiwa na jamii ya kimataifa. Mbunge mwingine wa Nairobi Tom Kajwang alikamatwa na kufikishwa mahakamai na hatimaye kuachiliwa kwa dhamana.
Mwanaharakati mwingine wa upinzani wakili Miguna miguna pia alikamatwa jana na angali anazuliwa na polisi licha ya mahakama kuruhusu kuachiliwa kwake kwa dhamana.
Bwana Aladwa alikamatwa siku ya Ijumaa usiku katika nyumba yake iliopo Buruburu kulingana na kiranja wa walio wachache bungeni Junet Mohamed.
Bwana Mohammed ambaye pia mbunge wa Suna Mashariki alisema kuwa bwana Aladwa kwa sasa anazuiliwa katika makao makuu ya ujasusi.
Polisi hawajatoa tamko lolote kuhusiana na kukamatwa kwa Aladwa.
KIONGOZI MWINGINE WA UPINZANI AKAMATWA NCHINI KENYA
Reviewed by By News Reporter
on
2/03/2018 02:21:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: