Loading...
Liliane Iradukunda amerithi taji la aliyekuwa Mrembo wa Rwanda mwaka 2017, Elsa Iradukunda kama Mrembo wa mwaka 2018.
Ameshinda taji la urembo mwaka 2018 katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Iconic Kigali Convention Centre Auditorium, Usiku wa jana Jumamosi.
Mrembo huyo amewashinda washindani wenzake 20. Iradukunda (18) ambaye alikuwa anawakilisha kanda ya Mashariki mwenye kilogramu 57 na urefu wa sentimita 170.
Iradukunda amejishindia taji la urembo na vitu vingine kama gari mpya aina ya Suzuki Baleno na kupewa mshahara wa 800,000 pesa za kinyarwanda kwa kipindi cha mwaka wote.
Alipokea zawadi ya nyongeza ya tiketi ya ndege kutoka katika kampuni RwandaAir atakayotumia kwenda katika mashindano ya urembo wa dunia.
Tuma neno 'BURUDANI' kwenda +255765112259 kupata habari za burudani punde zinapojiri.
LILIANE IRADUKUNDA ATWAA TAJI LA MISS RWANDA 2018
Reviewed by By News Reporter
on
2/25/2018 10:18:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: