Loading...

"MARUFUKU KUSHEREHEKEA SIKU YA WAPENDA NAO" - Meya wa Indonesa

Loading...
Meya wa Mataram, West Nusa Tenggara Barat nchini Indonesia amepiga marufuku kusherehekea Siku ya wapenda nao (maarufu, Valentine's Day) katika jiji hilo.

Amesema kwamba sio utamaduni wa nchi ya Indonesia ambao unapaswa kudumishwa.

Kusherehekea siku ya wapendanao sio utamaduni wetu,. Ndio maana tumekataza kuisherehekea-hususani kwa wanafunzi na mazingira ya shuleni, "Meya wa Mataram Ahyar Abduh alisema juzi, Jumatatu, Februari 12.

Meya huyo aliwaomba bodi ya shule kuwasisitiza wanafunza kuzingatia masomo zaidi.

Mkuu wa bodi za shule za Mataram, Chief. Sudenom alisema ilani hiyo ilishatangazwa toka mwanzoni mwa mwezi Februari na sio kwa wanafunzi tu, bali hata kwa wazazi wao na atakaye kiuka agizo hilo atagewa adhabu kali.

Na hakuweka ni adhabu itatolewa lakini itakuwa katika mtindo wa adhabu za kijamii-kwa kutangaza majini ya washukiwa wakati wa baraza la shule la asubuhi.

Na kwa wanafunzi watakaosherehekea siku ya wapenda nao nje ya muda wa shule, hiyo itakuwa ni wajibu wa wazazi wao.

"Tunaimani kwamba wazazi wanaweza kuwa sambamba na sisi na kuwakataza watoto wao kuadhimisha siku ya wapendanao," Sudenom alisema.
"MARUFUKU KUSHEREHEKEA SIKU YA WAPENDA NAO" - Meya wa Indonesa "MARUFUKU KUSHEREHEKEA SIKU YA WAPENDA NAO" - Meya wa Indonesa Reviewed by By News Reporter on 2/14/2018 09:38:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.