Loading...

SANAMU LA BOB MARLEY KUJENGWA NCHINI ZIMBABWE

Loading...
Mshauri wa maswala ya sanaa ya nchi ya Zimbabwe anatarajia kujenga sanamu la Bob Marley - Mfalme wa reggae katika Uwanja wa Rufaro mjini Harare, ambapo Bob alitumbuiza mwaka 1980 kuashiria uhuru katika nchi hiyo.

Tangazo hilo limekuja siku tatu baada ya kumbu kumbu ya kuzaliwa kwake tarehe 6 Februari - siku iliyosherehekewa nchini kwake Jamaica.

Martin Chemhere alifanya mazungumzo na mmiliki wa mali za Marley kuhusu ujenzi wa sanamu lake na inaonekana ameruhusu ujenzi huo.

Lakini kuna masharti: Sanamu hilo liwa kwa ajili ya umma na wapate ruhusa pia kutoka katika familia ya Marley.

Marley alikuwa na mahusiano mazuri sana na nchi ya zimbabwe na hata kuandika nyimbo kwa ajili kuunga mkono harakati za uhuru wa nchi hiyo.
SANAMU LA BOB MARLEY KUJENGWA NCHINI ZIMBABWE SANAMU LA BOB MARLEY KUJENGWA NCHINI ZIMBABWE Reviewed by By News Reporter on 2/10/2018 08:05:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.