Loading...
Ukiwa katika miezi ya awali ya mwaka mpya usisahau kuendelea kufanya tathmini ya mwenendo wa maisha yako ili kubaini kama uko katika uelekeo sahihi wa kufanikisha malengo uliyojiwekea.
Hakikisha kila siku unajitathmini, usijisahau ukaja kukumbuka tayari umeshapotea katika uelekeo uliokusudia mwanzo.
Nina amini wengi tumejiwekea malengo ya kukamilisha kwa mwaka huu, kama hujafanya hivyo bado una nafasi ya kutengeneza malengo yako yatakayokuongoza mwaka mzima.
Usithubutu kuishi bila kujiwekea malengo, ni hatari. Ni sawa na kutembea katika jangwa, muda wowote unapotea.
You Deserve The Best
Vicent Stephen
KILA SIKU ENDELEA KUTATHMINI MWENENDO WAKO ILI KUREKEBISHA MAKOSA
Reviewed by By News Reporter
on
2/06/2018 04:54:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: