Loading...

UHARIBIFU WA MAZINGIRA NI CHANZO CHA MIGOGORO NIGERIA

Loading...
Nigeria imekuwa ikikabiliwa na migogoro kati ya jamii za wafugaji (fulani) ambao wanaasili ya dini ya kiislamu na wafugaji wenye asili ya dini ya kikristo. Mwaka 2016 mgogro huwa ulisababisha vifo vya watu 2,500 na zaidi ya 62,000 kupoteza makazi yao na kuperekea kupoteza mapato zaidi ya dola za kimarekani bilioni 13.7, ikiwa mwezi Januari 2018 pekee, mgogoro huwa umesababisha vifo vya watu 168.

Kutoka na mgawanyiko wa kidini baina ya wahanga wa mgogoro huo, pale mapigano yanapoanza kutokea makanisa na misikiti uchomwa moto na hata kuuana kwa makundi hayo.

Kisichoangaziwa ni mtazamo wa mazingira. Nigeria ina eneo zaidi ya kilometa za mraba 1000 limepita jangwa la Sahara eneo lake la Kaskazini. Na jangwa hilo linajongea kuelekea kusini mwa Nigeria kwa kasi ya mita 600 kwa mwaka. Wakati huo huo, Ziwa Chad upande wa Kusini-Mashariki linaanza kukauka. Wafugaji wenye asili ya kabila la fulani wanaanza kuelekea kusini zaidi kutafuta malisho na kadri wanavyoelekea kusini basi wanaendelea kukutana na jamii ya wakulima ambao ni wakristo.

Kwahiyo chanzo kikubwa cha mgogoro huu ni Mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira na sio sababu za kidini zinazoangaziwa. Na ikiwa serikali ya nchi ya Nigeria itavunja ukimya na kuelekeza nguvu yake katika kuhakisha watu wa maeneo hayo wanatunza mazingira basi hakutakuwa na migogoro na kumaliza vifo vya raia wasio na hatia.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika punde zinapojiri.
UHARIBIFU WA MAZINGIRA NI CHANZO CHA MIGOGORO NIGERIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NI CHANZO CHA MIGOGORO NIGERIA Reviewed by By News Reporter on 2/26/2018 01:14:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.