Loading...
Wanafunzi watano wa kike nchini Kenya wafikishwa katika hospitali ya Embu baada ya kubakwa na wanaume 10 waliovamia kwenye mabweni yao huko Bondeni Estate, Embu siku ya Alhamisi usiku.
Wanafunzi katika Chuo cha Embu pia walipoteza thamani wakati kikundi cha watu wasiojulikana wenye silaha za hatari baada ya kuvamia katika mabweni yaliyo nje ya taasisi nyakati za usiku.
Mabweni ya Castle yapo mita 100 karibu na Embu West AP na inahudumia wanafunzi katika Chuo cha Embu na Chuo Kikuu cha Chuka.
Polisi Mkuu wa Kata ya Embu Nelson Okioga pamoja na Embu West OCPD Esther Muhoro walitembelea mabweni hayo kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo lililowashtua na kuwatia hofu wanafunzi.
Wanafunzi waliohojiwa juu ya tukio hilo walisema kikundi hicho cha watu wasiojulikana waliwatishia wanafunzi endapo watapiga kelele watawapiga na kuwaumiza vibaya.
Waliwateka kwa dakika kadhaa wakidai pesa na vitu vingine vya thamani, kabla ya kuwabaka.
Wanafunzi watano waliwaishwa katika hospitali ya Embu Level Five kwa matibabu ikiwa polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
"Wanafunzi wanahali mbaya lakini wanapata matibabu," alisema muuguzi katika kituo hicho.
Doris Mwende, mwanafunzi wa chuo cha Embu alisema tushawasilisha malalamiko yetu juu ya kuongezeka kwa matukio ya uhalifu hasa kwa wanafunzi wakike kuporwa na hata kujitokeza kwa matukio ya unyanyasaji wa kijinsi lakini tunapuuziwa.
WANAFUNZI WATANO WABAKWA NA GENGE LA WAHUNI NA KUFIKISHWA HOSPITALI
Reviewed by By News Reporter
on
2/05/2018 09:01:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: