Loading...
Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Zitto Kabwe ameachiliwa huru kwa dhamana asubuhi hii baada ya kukamatwa na polisi usiku wa kuamkia Februari 23mkoani Morogoro, karibu kilomita 200 kutoka Dar es salaam.
Sababu ikitajwa ni kufanya mikutano bila kibali alipokuwa akifanya ziara ya kutembelea viongozi wa chama chao cha ACT Wazalendo maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Alipokamatwa Bw Zitto aliweka ujumbe katika akaunti yake ya Twitter, "Ninasindikizwa hadi kituo cha polisi cha Mgeta wilayani, Mvomero.... Sijaambiwa kwa nini nimekamatwa."
bunge Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya shilingi milioni 50 fedha za kitanzania na kudhaminiwa na wakaili wake ndugu Emmanuel Lazarus Mvula.
Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo alikuwa kwenye ziara ya chama chake mkoani humo.
Ametakiwa kuripoti Polisi Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro Jumatatu, Machi12, 2018.
Baada ya kuachiwa kwa dhamana, Zitto Kabwe na viongozi wengine wa kitaifa wa chama hicho wamesema wataendelea na ziara ya kutembelea kata zinazoongozwa na chama hicho.
Vile vile Zitto akaelezea katika ukurasa wake wa Facebook " Baada ya kulala bure jana polisi Morogoro, tunaendelea na kazi yetu ya kutembelea kata zote ambazo Wananchi walitupa dhamana kwa kuchagua madiwani wa Act Wazalendo."
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kisiasa punde zinapojiri.

ZITTO KABWE AMEACHILIWA KWA DHAMANA, BAADA YA KUKAA JELA USIKU WA KUAMKIA JANA
Reviewed by By News Reporter
on
2/24/2018 11:44:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: