Loading...

ADUI NAMBA MOJA WA MAFANIKIO YAKO NI WEWE MWENYEWE - Na Siri ya Utajiri

Loading...
ADUI namba moja wa mafanikio yako ni WEWE mwenyewe. Kama kuna hali fulani huipendi katika maisha yako MTU wa kwanza kumlaumu ni WEWE binafsi. Watu wana tabia ya kulaumu wengine kuwa ndio chanzo cha matatizo yao huku wakisahau wajibu wao katika matatizo hayo.

Tunasema adui wa kwanza ni nafsi zetu kwa sababu tuna MAMLAKA ya kuruhusu au kutoruhusu hali fulani ya maisha tunayoishi. Kwa kiasi kikubwa hali yako ya sasa ni matokeo ya MAAMUZI yako na kama sivyo basi ni matokeo ya wewe kutofanya MAAMUZI stahiki.

Kufanikiwa ama kutofanikiwa mwanzo wake ni WEWE mwenyewe. Usikimbilie kutafuta sababu ya kwa nini hufanikiwi huku ukisahau nafasi na wajibu wako katika kuleta mafanikio katika maisha yako. Sisi wenyewe ndio kikwazo kutokana na MAWAZO yetu, MATENDO yetu, MATAMSHI yetu, TABIA zetu na MIENENDO yetu kwa ujumla.

Ni lazima tuwe tayari KUWAJIBIKA ili mambo yaweze kubadilika.

You Deserve The Best!
Vicent Stephen


Tuma neno 'UTAJIRI' kwenda +255765112259 kupata muendelezo wa makala za siri ya utajiri punde zinapojiri.
ADUI NAMBA MOJA WA MAFANIKIO YAKO NI WEWE MWENYEWE - Na Siri ya Utajiri ADUI NAMBA MOJA WA MAFANIKIO YAKO NI WEWE MWENYEWE - Na Siri ya Utajiri Reviewed by By News Reporter on 3/26/2018 02:39:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.