Loading...

DOGO JANJA AFUNGUKA RATIBA YA 'URODA' ALIYOPANGIWA NA UWOYA

Loading...

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo Janja ambaye ni mume halali wa muigizaji wa filamu bongo Irene Pancras Uwoya, ameweka wazi sababu za kupangiwa ratiba na mke wake huyo, jambo ambalo lilizua kizaa zaa baada ya kuiweka kwenye mtandao.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dogo Janja amesema alishtuka baada ya kuona ratiba hiyo imebandikwa ukutani alipoamka, na kueleza sababu zake.

“Nilikuwa nimelala nimeamka nikakutana na ratiba kwenye ukuta, nikaangalia duh!! nikaipost insta. Unajua yule ni mshkaji wangu sana alikuwa ananitania, na yeye ndiye alianza kuipost, na kimvua hiki uniambie ratiba!!? Atadondoka mtu”, amesema Dogo Janja

Wawili hao walifunga ndoa ya kimya kimya jambo ambao wengi hawaamni mpaka leo kuwa ni wanandoa, na pia kutokana na tofauti ambazo wanaonekana wanazo za kiumri.
Na Geofrey Okechi - Dar es salaam

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
DOGO JANJA AFUNGUKA RATIBA YA 'URODA' ALIYOPANGIWA NA UWOYA DOGO JANJA AFUNGUKA RATIBA YA 'URODA' ALIYOPANGIWA NA UWOYA Reviewed by By News Reporter on 3/17/2018 07:55:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.