Loading...

DONALD TRUMP KUTANGAZA VIKWAZO DHIDI YA CHINA

Loading...
Rais wa Marekani Donald Trump anajiandaa kutangaza vikwazo dhidi ya China katika kile alichokisema ni wizi wa haki miliki hatua ambayo imeamsha hofu ya vita vya kibiashara wakati huu utawala wa Beijing ukiapa kujibu mapigo.

Msemaji wa ikulu ya Marekani Raj Shah amesema kuwa rais Trump atatangaza vikwazo hivyo baada ya uchunguzi kuhusu taifa la China, kuharibu soko, shinikizo, kuiba teknolojia ya Marekani na wizi wa haki miliki.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ikulu Jumatano jioni imeonesha kuwa rais Trump atatia saini mkataba ambao utalenga nguvu ya uchumi wa China.

Hata hivyo Serikali ya Beijing nayo imejibu kwa kutoa taarifa kusisitiza kuwa nchi yao itachukua hatua stahili kulinda haki zake za kimsingi pamoja na maslahi yake kibiashara.

Hatua hii imekuja ikiwa ni majuma kadhaa yamepita tangu rais Trump atangaze kuchukua hatua zaidi dhidi ya mataifa ya kigeni yanayofanya biashara ya Chuma na Aluminium na nchi hiyo ambapo sasa wameongezewa ushuru wa forodha.

Hatua yake ilisababisha kujiuzuli kwa mshauri wake mkuu wa masuala ya uchumi Gary Cohn.

Siku ya Jumatano mwenyekiti wa hifadhi ya taifa Jerome Powell alionya kuwa vita ya kibiashara inaendelea kukua na kuwa tishio kwa uchumi mkubwa wa dunia.

Waziri mkuu wa China Li Keqiang alitoa wito kwa rais Trump kutofanya maamuzi kwa kutumia hisia lakini kiongozi huyo ameendelea kutooonesha ishara ya kurudi nyuma kutokana na maamuzi yake.

Hivi karibuni Marekani imesema kuwa watapata kiasi cha dola za Marekani milioni 30 kutokana na ushuru utakaotokana na uagizaji wa bidhaa kutoka China.

Rais Trump ameonekana kuridhika na kiasi hiki kitakachopatikana katika kujaribu kutimiza ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni ya kulinda viwanda vya ndani na udanganyifu unaofanywa na wapinzani wake kiuchumi akisema hatua yake itattengeneza ajira zaidi kwa Wamarekani.

Marekani imekuwa ikiituhumu China kuyalazimisha makampuni ya Marekani kutoa haki za kibiashara na haki miliki zake ili yaweze kufanya kazi na kutoa huduma nchini humo.
Na Geofrey Okechi

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.
DONALD TRUMP KUTANGAZA VIKWAZO DHIDI YA CHINA DONALD TRUMP KUTANGAZA VIKWAZO DHIDI YA CHINA Reviewed by By News Reporter on 3/23/2018 08:29:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.