Loading...

HII NDIO SABABU YA KUFUTWA KWA MICHEZO SITA LEO KATIKA LIGI YA SERIE A - ITALI

Loading...
Nahodha wa klabu ya soka ya Fiorentina nchini Italia Davide Astori amefariki dunia usiku wa jana kabla ya mchuano wa timu yake dhidi ya Udinese.

Klabu hiyo ya mjini Florence imethibitisha kifo hicho. Kufuatia kifo hicho michezo yote sita ya Serie A iliyotarajiwa kuchezwa hii leo imefutwa, na tarehe mpya ya michezo hiyo itapangwa hapo baadaye. 

Imeelezwa kuwa mshituko wa moyo unaweza kuwa chanzo cha kifo cha mchezaji huyo mwenye miaka 31 ambaye alikuwa akicheza msimu wake wa tatu akiwa na klabu hiyo inayojulikana pia La Viola.

Wachezaji wenzake Astori waliripotiwa kumkuta nahodha huyo akiwa katika chumba cha hoteli mjini Udine ambako kikosi cha Fiorentina kilifikia jana Jumamosi, ambapo hakuweza kuamka tena kutoka katika usingizi aliolala toka ijumaa usiku.

Tuma neno 'MICHEZO' kwenda +255765112259 kupata habari za michezo punde zinapojiri.
HII NDIO SABABU YA KUFUTWA KWA MICHEZO SITA LEO KATIKA LIGI YA SERIE A - ITALI HII NDIO SABABU YA KUFUTWA KWA MICHEZO SITA LEO KATIKA LIGI YA SERIE A - ITALI Reviewed by By News Reporter on 3/04/2018 10:40:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.