Loading...

IS WASAMBAZA VIDEO ZA MAUAJI YA WANAJESHI WA MAREKANI

Loading...
Wapiganaji wa kundi la Islamic State IS wamesambaza picha za video zinazodaiwa kuonyesha mauaji ya wanajeshi wane wa Marekani waliouawa nchini Niger mwezi Octoba mwaka mwaka jana.

Hata hivyo haijajulikana mara moja kwanini picha hizo zimetolewa kwa kuchelewa hadi, ambapo zimetolewa kupitia program ya kimtandao ya Telegram

Picha hizo zilipigwa na mmoja wa wanajeshi wa Marekani kupitia kamera yake ya siri aliyokuwa nayo kwenye kofia yake ngumu aliyokuwa ameivaa yaani Helmet.

Lengo la video hizo ni kutaka kubainisha kwamba IS ndiyo waliofanya shambulio hilo.

Picha zinazo onekana zinaanza na zile za mnato ambazo baadhi ya wapiganaji hao wakitoa kiapo cha utii kwa kiongozi wao Abu Bakr al-Baghdadi mtandao huo wenye makundi yenye utiifu kwa IS kama vile Sahel, Jamaat Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM).

Kwa mjibu wa mtandao wa BBC video hizo zinawaonyesha wapiganaji hao wakitembea na kukimbia jangwani kuelekea kufanya shambulizi.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.
IS WASAMBAZA VIDEO ZA MAUAJI YA WANAJESHI WA MAREKANI IS WASAMBAZA VIDEO ZA MAUAJI YA WANAJESHI WA MAREKANI Reviewed by By News Reporter on 3/05/2018 09:43:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.