Loading...

JAJI MKUU MSTAAFU MOHAMMED CHANDE ATEULIWA NA UN KUCHUNGUZA KIFO CHA ALIYEKUWA KATIBU MKUU UN

Loading...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, (UN), Antonio Guterres amemteua Jaji Mkuu mstaafu  wa Tanzania, Mohammed Chande Othman kuongoza jopo la  uchunguzi wa kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa UN, Dag Hammarskjöld.

Hammarskjold aliyekuwa katibu mkuu wa pili wa UN alifariki dunia Septemba 18 1961 katika ajali ya ndege iliyotokea huko Ndola, Zambia, wakati akiwa katika safari ya kikazi ya kuhamasisha amani Zaire, kwa sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Uteuzi wa Jaji Othman huo ni kwa mujibu wa azimio namba 72/252, la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na uteuzi huo unajumuisha jopo la wajumbe aliokuwa nao awali.

Uteuzi huo unatokana na ripoti iliyowasilishwa na Baraza Kuu la UN ambalo lilibaini kuwa pamoja na mambo mengine, sababu kuu ya kuanguka kwa ndege hiyo ni shambulizi la nje au vitisho vilivyosababisha ndege hiyo ianguke.

Taarifa ya UN, imewataka nchi wanachama kumpa ushirikiano Jaji Chande wakati akitekeleza majukumu yake, ikiwamo kumpa taarifa zinazoweza kumsaidia katika uchunguzi wake.
Na Neema Joshua.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kitaifa punde zinapojiri.
JAJI MKUU MSTAAFU MOHAMMED CHANDE ATEULIWA NA UN KUCHUNGUZA KIFO CHA ALIYEKUWA KATIBU MKUU UN JAJI MKUU MSTAAFU MOHAMMED CHANDE ATEULIWA NA UN KUCHUNGUZA KIFO CHA ALIYEKUWA KATIBU MKUU UN Reviewed by By News Reporter on 3/29/2018 09:42:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.