Loading...

KAMWE USIACHE ULICHOKIANZISHA KAMA UNATAKA KUFANIKIWA - Na Siri ya Utajiri

Loading...
Moja ya  changamoto kubwa inayorudisha nyuma jitihada za watu kufikia malengo yao ni MUENDELEZO wa kile WALICHOKIANZISHA. Watu wengi wameanzisha vitu vizuri kama hatua ya mwanzo kabisa lakini wameshindwa kuendelea zaidi ya hatua ya mwanzo.

Unakuta mtu anakuwa na HAMASA na NGUVU za kuanza lakini baada ya siku chache hamasa hiyo inatoweka na kidogo kidogo anaanza kupoteza UELEKEO na kuachana na jambo ambalo alikuwa amelianzisha.

Mawazo mazuri yamepotea kwa watu kushindwa kuyaendeleza. Kipimo cha MAFANIKIO si katika kuanza tu bali pia katika KUSIMAMIA kile ulichokianzisha na kuhakikisha UNAENDELEA kuchukua hatua kila siku hadi ufike sehemu uliyokuwa umekusidia.

Kama wewe ni mmoja wa watu walioanzisha jambo kisha wakaachia njiani leo nenda kafufue jambo hilo. Mbegu lazima imwagiliwe maji kila siku ili iweze kuchanua. Kuna mafanikio makubwa mbele ya safari yako, usiishie njiani. Endelea!

You Deserve The Best!
Vicent Stephen

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
KAMWE USIACHE ULICHOKIANZISHA KAMA UNATAKA KUFANIKIWA - Na Siri ya Utajiri KAMWE USIACHE ULICHOKIANZISHA KAMA UNATAKA KUFANIKIWA - Na Siri ya Utajiri Reviewed by By News Reporter on 3/15/2018 12:36:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.