Loading...

KUNDI LA NYANI LAHAMISHA WATU MAKAZI

Loading...
Wakazi katika jamii ya  wa Soluyi/Sosanya huko Gbagada, Lagos - Nigeria, imeripotiwa kulazimishwa kuyahama makazi yao baada ya kuvamiwa na idadi kubwa ya nyani katika jamii yao.

Kwa mujibu wa wakazi hao, nyani hao waliingia mazingira wanayoishi kwa na kuanza kuvunja madirisha na kuanza kuingia vyumbani na kuanzia kula vyakula na vitu vingine. Adigun Olaleye, Mwenyekiti wa Jumuia na Umiliki wa Makazi, alisema uvamizi wa wa nyani hao pengine umesababishwa na ukaribu wa wakazi hao kuwa karibu na msitu ambao unatenganisha jamii hiyo na eneo la Ifako.

Olaleye alisema kwamba nyani hao wanaingia katika majumba ya watu wakati wowote hata kama nyumba zao zimefungwa. Kilichoperekea kuwachanganya wana habari, wakazi wa eneo hilo wamedai kwamba ni vigumu kwa wao kuendelea kuishi hapo kwa hali hiyo inayoendelea.
Na Geofrey Okechi.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za matukio punde zinapojiri.
KUNDI LA NYANI LAHAMISHA WATU MAKAZI KUNDI LA NYANI LAHAMISHA WATU MAKAZI Reviewed by By News Reporter on 3/27/2018 08:07:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.