Loading...

KUWAIT KUISUKA MNAZIMMOJA-ZANZIBAR KWA 31bl/-

Loading...
SERIKALI ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 207.3, sawa na shilingi bilioni 466.4, kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko wa kuingia katikati ya mji wa Dodoma pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma, yenye urefu wa kilometa 257.

Ahadi hiyo imetolewa mjini Dodoma na Balozi wa Kuwait nchini, Jassem Ibrahim Al-Najem, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango.

Balozi Al-Najem alisema mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na kutoka mjini Dodoma zitasaidia kuondoa msongamano wa gari zinazopita katikati ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya makao makuu ya serikali kuhamia mjini humo.

Aliahidi kuwa nchi yake kupitia mfuko huo, iataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa ufadhili wa ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu na kilimo ili iweze kukuza uchumi na maisha ya watu wake.

Katika kipindi cha miaka 40, Serikali ya Kuwait, imeipatia Tanzania mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 608 kwa ajili ya kutekeleza miradi 14 ya kiuchumi katika sekta za barabara, kilimo, umeme, maji na afya.

Baadhi ya miradi hiyo ambayo imekamilika ni pamoja na barabara ya Dar es Salaam hadi Somanga inayohusisha pia ujenzi wa daraja la Mkapa, kiwanda cha karatasi Mufindi, mradi wa kuzalisha umeme unaotokana na nguvu ya maji-Mtera, na gharama za upembuzi yakinifu wa upanuzi wa bandari ya Zanzibar.

Kwa upande wake, Waziri Mpango, aliishukuru serikali ya Kuwait kwa kuisaidia Tanzania kutimiza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia mikopo yenye gharama nafuu inayotolewa na taasisi hiyo.

Alisema mwaka jana, Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait uliipatia Tanzania mkopo nafuu wa shiingi bilioni 115 kwa ajili ya kuimarisha  barabara ya Chaya hadi Nyahua (km 85) kwa kiwango cha lami pamoja na mradi wa maji safi na salama wa miji ya Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro na sehemu ya eneo la wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wenye thamani ya shilingi bilioni 77.

Mradi mwingine ni ufadhili wa matengenezo ya hospitali ya Mnazimmoja-Zanzibar utakaogharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 13.6 sawa na shilingi bilioni 31.
Na Mohammed Makame - Zanzibar.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kitaifa punde zinapojiri.
KUWAIT KUISUKA MNAZIMMOJA-ZANZIBAR KWA 31bl/- KUWAIT KUISUKA MNAZIMMOJA-ZANZIBAR KWA 31bl/- Reviewed by By News Reporter on 3/25/2018 11:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.