Loading...

MCHUNGAJI ALIYEJARIBU KUMFUFUA MFU AKAMATWA NA POLISI

Loading...
Muhubiri/Mchungaji mmoja nchini Msumbiji amejipata mikononi mwa polisi baada ya kujaribu kumfufua mwanamume mmoja eneo la kati la Msumbiji bila mafanikio

Mchungaji huyo alidai kuwa roho mtakatifu alimwambia alisafiri hadi katika hospitali ya Chimoio katika jimbo la Manica, kufanya muujiza huo.

Mchungaji huyo ambaye aliyedai kuwa na uwezo wa kufanya mwujiza huo aliweza kuikonga mioyo ya maafisa wa hospitali hadi wakamruhusu aingie ndani ya chumba cha maiti kuutekeleza muujiza wake.

Hata hivyo baada ya siku mbili za maombi makali, hakuweza kabisa kurejesha uhai wa marehemu.

Haikuishangaza familia ya marehemu.

Dada yake marehemu - ambaye hakutaka jina lake litajwe - aliwaambia waandishi wa habari:

"Mchungaji aliomba, akaomba na kuomba hadi akanena kwa lugha. Alizungusha kichwa cha marehemu huku na kule huku akiomba.

"Lakini hakuna hata sehemu ya marehemu kaka yangu iliyoweza kutikisika. Wakati mmoja mchungaji alipaza sauti akisema: 'amka, kijana wa Mungu!"

"Hatukuamini mchungaji angefanya mwujiza wowote. Hii ni kwa sababu hakuwahi, hata wakati mmoja, kuthibitisha uwezo wake wa kumrejeshea mfu uhai wake.

"Tangu wakati huo kasisi alikamatwa na yuko mikononi mwa polisi akishtakiwa kwa kosa la kumkosea heshima mfu."
Na Fatma Pembe.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
MCHUNGAJI ALIYEJARIBU KUMFUFUA MFU AKAMATWA NA POLISI MCHUNGAJI ALIYEJARIBU KUMFUFUA MFU AKAMATWA NA POLISI Reviewed by By News Reporter on 3/29/2018 11:43:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.