Loading...

MNENGUAJI ZODWA WABANTUA AZUIWA KUTUMBUIZA NCHINI ZAMBIA

Loading...
Zambia yamzuia mnenguaji na mtumbuizaji Zodwa Wabantu anayechezwa kwa mtindo wa kuchuchumaa kutumbuiza nchini humo kwa sababu ya kulinda maadili.

Waziri wa Maadili na Maswala ya Kidini Godfridah Sumaili aliiambia gazeti la The Time la Zambia kwamba serikali haitoruhusu Zodwa "kutumbuiza mahali popote nchini".

"Iko wazi kuwa sisi ni nchi yenye maadili ya Kikristo na tunapaswa kuheshimu na kulinda maadili na miiko... kama taifa, hatuwezi kuruhusu hilo. Namaana kwa mtu kutumbuiza bila chupi, hakuna maadili hapo," imenukuliwa alivyosema.

Zodwa ni mnenguaji machachari, ambaye maarufu sana huko Afrika ya Kusini kwa kucheza kwa mtindo wa kuchuchumaa bila ya chupi.

Alitakiwa kutumbuiza mjini Lusaka mwisho wa juma lililopita wakati wa uzinduzi wa albamu ya msanii Karasa Karayo inayokwenda kwa jina la Pandemonium.

Uamuzi wa kumzuia mnenguaji huyo umezua malumbano huko mitandaoni ikiwa baadhi ya Wazambia wakilaumu serikali na kusema ni kuishusha tasania ya burudani.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
MNENGUAJI ZODWA WABANTUA AZUIWA KUTUMBUIZA NCHINI ZAMBIA MNENGUAJI ZODWA WABANTUA AZUIWA KUTUMBUIZA NCHINI ZAMBIA Reviewed by By News Reporter on 3/13/2018 08:18:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.