Loading...

NIGERIA MBIONI KURUHUSU BANGI ITUMIKE KAMA DAWA

Loading...
Ishara kubwa imeonekana siku ya Jumatatu kwamba nchi ya Nigeria ipo mbioni kulegeza sheria juu ya matumizi ya mmea wa 'bangi', kwa madai ya kuwa Umoja wa Mataifa imethibitisha matumizi ya mmea huo kama utumike kama tiba.

Lakini Umoja wa Mataifa kupitia mwakilishi wake Afisa wa Mradi wa maswala ya Dawa na Uhalifu huko Nigeria, Harsheth Kaur Vir alisema ni lazima nchi ya Nigeria izuie vijana wasitumie mmea huo kwa matumizi ya kujistarehesha ijapokuwa wanapendekeza utumike kama tiba.

Kwa mujibu wa Afisa huyo, alisema Mmea wa bangi ni dawa ya ajabu ambao umeruhusiwa kwa matumizi ya dawa, lakini sio kujistarehesha, "Nigeria ni nchi ambayo imeweka sheria kali juu ya matumizi ya mmea huo kama dawa za kulevya lakini UN imeruhusu utumike kama dawa baada ya kufanyika tafiti na taasisi ya kimataifa ya madawa", aliongezea.
Na Geofrey Okechi.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika punde zinapojiri.
NIGERIA MBIONI KURUHUSU BANGI ITUMIKE KAMA DAWA NIGERIA MBIONI KURUHUSU BANGI ITUMIKE KAMA DAWA Reviewed by By News Reporter on 3/27/2018 10:33:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.