Loading...

PAUL BIYA: RAIS WA CAMEROON ANAYEONGOZA 'KUSAFIRI NJE'

Loading...
Rais wa Cameroon Paul Biya amekuwa madarakani kwa takriban miaka 35. Lakini utawala wake wa miaka mingi umekuwa gumzo nyumbani , muda anaotumia akiwa katika mataifa ya kigeni umezua hisia za kimataifa.

Kutokuwepo kwake katika taifa hilo kumewafanya wakosoaji wake kutoa hisia kali dhidi yake.

Safari zake za kigeni zimesababisha makabiliano ya mtandaoni kati ya gazeti la Tribune na mradi wa uhalifu unaopangwa na Ufisadi OCCRP ambao ulihesabu muda unaotumiwa na rais huyo ugenini kwa kutumia ripoti za magazeti ya kila siku.

Mradi huo wa kukabiliana na ufisadi na ripoti za uhalifu unakadiria kwamba rais alitumia takriban siku 60 nje ya taifa hilo mwaka uliopita katika ziara za kibinafsi.

Pia imedaiwa kwamba alitumia thuluthi moja ya mwaka 2006 na 2009 ughaibuni.

Hoteli ya Intercontinental mjini Geneva ndio imedaiwa kuwa anayoipenda. Gazeti hilo linalomilikiwa na serikali lilitaja uchunguzi uliofanywa kuwa propanganda za uchaguzi.

Nyumbani, rais amekuwa haonekani hadharani na mara nyengine huelekea nyumbani kwake mashambani.

Huamini uongozi wa kila siku serikalini wa waziri wake mkuu Philemon Yang ambaye hufanya mikutano ya kila mwezi ya baraza la mawaziri. Waziri huyo mkuu hupewa uwezo mkubwa wa kusimamia kazi za kundi lake la mawaziri huku rais huyo akikutana na viongozi wakuu kibinafsi katika makao ya rais katika mji mkuu wa Younde.

Mtindo wa rais Biya kuliongoza taifa hilo akiwa ughaibuni umewafanya wakosoaji wake kuzungumza kuhusu ''rais anayeongoza akiwa ugenini''.

Hivyobasi rais huyo anayeongoza kutoka ughaibuni amekuwa akionyesha uthabiti wa uongozi wake huku akijiandaa kuachilia madaraka.
Na Geofey Okechi.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika punde zinapojiri.
PAUL BIYA: RAIS WA CAMEROON ANAYEONGOZA 'KUSAFIRI NJE' PAUL BIYA: RAIS WA CAMEROON ANAYEONGOZA 'KUSAFIRI NJE' Reviewed by By News Reporter on 3/26/2018 08:18:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.