Loading...

RAIS MPYA WA ZIMBABWE MNANGAGWA AMJIBU MUGABE

Loading...
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema nchi hiyo imeshapiga hatua baada ya kumwondoa madarakani kiongozi wa zamani Robert Mugabe.

Kauli hii imemjibu Mugabe ambaye kwa mara ya kwanza alijitokeza na kusema hatua ya kumwondoa madarakani ilikuwa ni kumpindua kijeshi.

Mugabe alisema alishangazwa sana na hatua ya Mnangagwa ambaye alimsadia kumwingiza kwenye ulingo wa kisiasa, ambaye sasa amembadilikia.

Hata hivyo, Mnangagwa amesema rais Mugabe ana haki ya kusema anachotaka kama raia yeyote wa kawaida.

“Taifa letu limeshapiga hatua. Lengo letu sasa ni kuandaa Uchaguzi Mkuu mwaka 2018,” alisema Mnangagwa.

Uchaguzi utafanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Na Catherine Kisese - Dar es salaam
RAIS MPYA WA ZIMBABWE MNANGAGWA AMJIBU MUGABE RAIS MPYA WA ZIMBABWE MNANGAGWA AMJIBU MUGABE Reviewed by By News Reporter on 3/17/2018 08:58:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.