Loading...

RAPPA RICK ROSS MAHUTUTI KITANDANI LAKINI '50 CENT' HAJAACHA KUMTUPIA VIJEMBE

Loading...
Kufuatia na msanii Rick Ross kufikishwa hospitalini, rappa 50 cent alipost picha ya kipande cha video kilichochezwa katika filamu ya 'Rocky IV' kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo muigizaji alisema, 'Kama atakufa, na afe tu.' Anaonekana akimtupia vijembe msanii mwenzake huyo mwenye bifu naye kwa kipndi kirefu sana.

Kawaida watu hutuma ujumbe au maua mazuri endapo mtu ameugua gafla, lakini kwa msanii 50 cent (42) imekuwa tofauti inaonekana ana njia tofauti ya kumfikia mgonjwa. Baada ya habari kuenea kote kwamba msanii Rick Ross (42) amefikishwa hospitalini kwa 'Mshtuko wa Moyo', mwimbaji wa "In Da Club" alipost picha kwenye ukurasa wake wa instagram ikionekana kama ni kejeli kubwa kwa msanii mwenzake.

Picha hiyo ilionyesha picha ya muigizaji 'Dolph Lundgren' alipokuwa katika kipande hicho cha video kama Ivan Drago akisema "Kama atakufa na afe tu" wakati akiwa pembeni ya adui wake Apollo Creed. Je, huo ni ujumbe ambao rappa 50 cent alijaribu kumtumia adui wake wa kipindi kirefu? Kama ndivyo. Hebu angalia ujumbe huo mwenyewe na utoe mtazamo wako.
Rick Ross alifikishwa hospitalini mapema Machi 1 baada ya mtu mmoja katika nyumba yake ya Miami kuwapigia simu polisi kupitia '911' akisema kunamtu "anaumwa vibaya sana, anapumua kwa shida na hajitambui." Baada ya kufikishwa hospitali, aliperekwa kwa wagonjwa mahututi na kuwekewa mipira ya kupumulia, ikimaanisha hajitambui na pia amewekewa mashine ili kumsaidia kupumua na kuendesha moyo wake.

Familia yake na watu wengine wa karibu, akiwemo mmoja wa mama watoto wake, walifika hospitalini hapo ili kumuona na kujua kinachoendelea. Na bado anaendelea kwa matibabu na anaendelea vizuri japo bado hajatoka chumba cha mahututi.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
RAPPA RICK ROSS MAHUTUTI KITANDANI LAKINI '50 CENT' HAJAACHA KUMTUPIA VIJEMBE RAPPA RICK ROSS MAHUTUTI KITANDANI LAKINI '50 CENT' HAJAACHA KUMTUPIA VIJEMBE Reviewed by By News Reporter on 3/04/2018 08:33:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.