Loading...
Mamlaka ya Serikali za Mtaa imesimamisha shughuli za kidini kwa makanisa 714 katika sehemu mbali mbali jijini Kigali, Rwanda kwa kushindwa kukidhi vigezo.
Sehemu za kufanyia ibada zimekutwa na upungufu wa miundo mbinu kama maliwato na sehemu za kutupia taka, viwango vya usalama na vibali kiujumla.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Vyama vya Siasa na Maswala ya Kijamii, Bw. Justus Kangwagye alidai kwamba sehemu za kufanyia ibada zinatakiwa kukidhi vigezo vya msingi kwa vipengele vya usalama, usafi, miundo mbinu na uhalali wa kisheria. Na kukosekana kwa vigezo hivyo ni kuhatarisha afya na usalama wa waumini.
Akifanyiwa mahojiano na kituo kimoja cha habari mjini Kigali, alisema: "Makanisa yote ambayo hayana vigezo hivyo alivyovitaji yalifungwa mara moja mpaka watakapo timiza masharti hayo"
Aliongezea, Makanisa mengine hayawezi kuanza na ibada mara moja kwa kuwa hata usajili wa kisheria hawajafanya mpaka sasa.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
SAFISHA JIJI YA MAKANISA ZAIDI YA 700 YAFANYIKA MJINI KIGALI
Reviewed by By News Reporter
on
3/01/2018 02:30:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: