Loading...

TAFITI ZINASEMA, UNYWAJI WA KAHAWA UNARAHISISHA MZUNGUKO WA DAMU MWILINI

Loading...
Wanasayansi wamegundua kuwa unywaji wa kahawa unasaidia mzunguko wa haraka wa damu kwa kusafisha kalsiamu katika mishipa.

Kulingana na habari za "The Telegraph", wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Brazil cha Sao Paulo wamechunguza mpango wa lishe na kiwango cha kalsiamu ya kwenye mishipa ya wafanyabiashara karibu 4,400 wa kahawa.

Kwa mujibu wa habari, utafiti huo umeonyesha kuwa wanywaji wa kahawa wana kiwango kidogo cha kalsiamu katika mishipa yao na mzunguko mzuri wa damu.

Hata hivyo wanasayansi wameonya kuwa ni vizuri kutozidisha vikombe vitatu vya kahawa kwa siku.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la "American Heart Association".
Na Catherine Kisese.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za afya punde zinapojiri.
TAFITI ZINASEMA, UNYWAJI WA KAHAWA UNARAHISISHA MZUNGUKO WA DAMU MWILINI TAFITI ZINASEMA, UNYWAJI WA KAHAWA UNARAHISISHA MZUNGUKO WA DAMU MWILINI Reviewed by By News Reporter on 3/31/2018 04:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.