Loading...

TAMASHA LA FILAMU LA URUSARO KUANZA RASMI MACHI 3, MJINI KIGALI

Loading...
Waigizaji na wataarishaji wa filamu wa kimataifa wanatarajiwa kushiriki katika msimu wa tatu wa Tamasha la Filamu la Wanawake la Kimataifa la Urusaro kuanzia mwezi Machi 3 hadi 9 katika hoteli ya Umubano, Kigali.

Inakidokezo cha "Sinema za kuwawezesha wanaweka", Tamasha hilo la kila mwaka limekuwa jukwaa maalumu la kuwaunganisha wacheza filamu, watayarisha filamu na watengeneza filamu ndani na nje ya Rwanda ili kuweza kubadilishana uzoefu katika tasnia ya filamu.

Tamasha hili kwa mara ya kwanza lilifanyika mwaka 2016 na waandaaji wa tamasha walikuwa 'Cine Femme Rwanda', shirika ambalo linawaunganisha pamoja waigizaji wajuzi wakike wa nchi ya Rwanda.

Jacqueline Murekeyisoni, Mwandaaji wa tamasha hilo, alisesema tamasha hilo ni fursa ya kuwaweka pamoja wanawake kubadilishana ujuzi ni jinsi gani watakuza tasnia ya filamu kutoka hatua moja na kwenda nyingine.

Tamasha la Mwaka huu, Murekeyisoni alisema, litakuwa tofauti kwa kuwa wanaangalia namna ya kuzindua "Siku ya Filamu nchini Rwanda" na kuisherekea siku moja na siku ya wanawake nchini Rwanda.

Siku ya tamasha, jumla ya filamu 15 kutoka nchi tofauti, 11 za nyumbani na nne za kigeni zinategemewa kutazamwa.

Tamasha hilo linatarajiwa kuwavuta watayarishaji wa filamu wanawake kutoka sehemu mbali mbali barani Afrika na nje ya bara, ikiwemo Nigeria, Burkina Faso, Gabon, Tanzania, Senegal, Tunisia, Ghana, France na USA.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za burudani punde zinapojiri.
TAMASHA LA FILAMU LA URUSARO KUANZA RASMI MACHI 3, MJINI KIGALI TAMASHA LA FILAMU LA URUSARO KUANZA RASMI MACHI 3, MJINI KIGALI Reviewed by By News Reporter on 3/01/2018 05:00:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.