Loading...

TRUMP AMSIFU RAIS WA CHINA KWA KUTAKA KUBAKIA MADARAKANI KWA MUHULA MWINGINE

Loading...
Rais wa Marekani Donald Trump amempongeza Rais wa China Xi Jinping kwa hatua aliyoichukua hivi karibuni ya kuhakikisha anasalia madarakani.

Katika hotuba aliyoitoa mjini Florida katika mkutano wa wahisani wa chama cha Republican, Trump anaripotiwa kusema kuwa Xi sasa ni Rais wa kudumu na anadhani hilo ni jambo zuri.

Kulingana na kituo cha televisheni cha CNN ambacho kimesema kilipata taarifa za yaliyojiri katika mkutano huo wa faragha wa Republican uliofanyika katika makazi ya Trump ya Mar-a-Lago, Trump anasemekana kufurahishwa na hatua hiyo ya Xi na kuongeza kuwa huenda wakati ujao nao wakachukua mkondo huo.

Chama tawala cha Kikomunisti nchini China mwezi uliopita kilipendekeza kuondolewa kwa mihula miwili ya Rais kuhudumu madarakani, pendekezo ambalo linatarajiwa kuidhinishwa na bunge hapo kesho Jumatatu katika kikao cha kila mwaka.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.
TRUMP AMSIFU RAIS WA CHINA KWA KUTAKA KUBAKIA MADARAKANI KWA MUHULA MWINGINE TRUMP AMSIFU RAIS WA CHINA KWA KUTAKA KUBAKIA MADARAKANI KWA MUHULA MWINGINE Reviewed by By News Reporter on 3/04/2018 09:25:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.