Loading...

TUADHIMISHE SIKU YA WANAWAKE KWA KUFAHAMU HILI: UTAFITI UMEONYESHA WANAWAKE WANA UWEZO MKUBWA WA KUKABILIANA NA HALI NGUMU

Loading...
Utafiti umeonyesha wanawake wana uwezo mkubwa wa kukabiliana na hali ngumu ukilinganisha na wanaume.

"Wanawake ni sugu zaidi kuliko wanaume hata katika hali mbaya zaidi, kama vile njaa na magonjwa."

Kwa mujibu  wa habari, utafiti huo umeelezewa katika gazeti la "Proceedings of the National Academy of Sciences" na kusema kuwa wanawake wana uwezo mkubwa wa kukabiliana na hali ngumu ukilinganisha na wanaume.

Katika utafiti uliofanywa na Virginia Zarulli kutoka katika chuo cha kusini mwa Denmark na James Vaupel kutoka katika chuo cha Duke nchini Marekani,watafiti hao wamefanya utafiti kuhusu maisha ya watu walioishi miaka 250 nyuma na kukabiliana na njaa pamoja na magonjwa mbalimbali.

Wametizama takwimu zote za vifo vilivyosababishwa na sababu hizo na ikaonekana kuwa wanawake wana uwezo mkubwa wa kujimudu.

Historia pia imeonyesha kuwa wanawake huishi maisha marefu ukilinganisha na wanaume.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kijamii punde zinapojiri.
TUADHIMISHE SIKU YA WANAWAKE KWA KUFAHAMU HILI: UTAFITI UMEONYESHA WANAWAKE WANA UWEZO MKUBWA WA KUKABILIANA NA HALI NGUMU TUADHIMISHE SIKU YA WANAWAKE KWA KUFAHAMU HILI: UTAFITI UMEONYESHA WANAWAKE WANA UWEZO MKUBWA WA KUKABILIANA NA HALI NGUMU Reviewed by By News Reporter on 3/08/2018 03:00:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.