Loading...

USAFIRI WA RELI KATI YA DRC NA ANGOLA WAANZA TENA

Loading...
Usafiri wa reli kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Angola umeanza tena baada ya kusitishwa kwa miaka 34 iliyopita, kwa sabbau ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Angola.

Hii ni hatua kubwa itakayosaidia sana kuimarika kwa biashara kati ya nchi hizo jirani, hasa wakati wa usafirishaji wa madini.

Uzinduzi huo umeshuhudia kontena 50 za mizigo zikitoka katika mji wa mpaka wa Dilolo Kusini Mashariki mwa DRC kuelekea kuelekea bandari ya Lobito nchini Angola.

Reli hiyo kati ya mji wa Lobito nchini DRC na Luau ilijengwa upya kwa usaidizi wa serikali ya China na kuzinduliwa rasmi mwezi Februari mwaka 2015.

Kabla ya kuwepo kwa reli hii, nchi hizo mbili zilikuwa zinatumia usafiri wa barabara kupitia nchini Zambia kusafirisha bidhaa mbalimbali.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika punde zinapojiri.
USAFIRI WA RELI KATI YA DRC NA ANGOLA WAANZA TENA USAFIRI WA RELI KATI YA DRC NA ANGOLA WAANZA TENA Reviewed by By News Reporter on 3/09/2018 10:35:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.